Thursday, August 3, 2017

AFYA NI NINI?

Afya ni hali ya kujisikia vizuri kimwili, kiakili, kiroho na kiutu pia, bila kusumbuliwa na ugonjwa wowote.
Afya ya binadamu itakuwa njema kama atafuatilia kanuni na taratibu bora za afya. Hiyo inajumuisha mlo kamili, yaani chakulachenye virutubisho vyote, vikiwemo protiniwanga na fati (hiyo iwe katika asilimia ndogo sana).
Pia anatakiwa awe safi kimwili na kimazingira, kama vile kwa kuoga na kusafisha mazingira yanayomzunguka.
Pia tunatakiwa kuwa na afya ya kiroho yaani kuishi kadiri ya mafundisho ya Mwenyezi Mungu kama vile: kupendana, kuthaminiana na kuacha dhambi: mara nyingi hizo (dhambi)  zinadhuru afya ya mwili pia.

No comments:

Post a Comment