UTI (Urinary Tract Infection):
v Ugonjwa Hatari unaoweza kuharibu FIGO na KIBOFU.

Maambukizi Katika Njia ya Mkojo (UTI) ni moja kati ya
magonjwa ambayo hayapewi msisitizo wa kutosha katika jamii licha ya kuwa wengi huathirika kwa ugonjwa huu bila kujua chanzo, tiba na kinga yake.
Ugonjwa huu huanza kuathiri mirija inayopitisha mkojo, baadaye huenea katika kibofu na figo. Mgonjwa anaweza kupata ugonjwa sugu wa figo na kupoteza maisha kama ugonjwa huu hautatibiwa mapema............
UTI husababishwa na vimelea ambao huingia kupitia mirija inayosafirisha mkojo na kuutoa nje. Vimelea hawa wanashambulia kibofu na baadaye huendelea mpaka kwenye figo. Hii ndiyo hatua kubwa ya ugonjwa ambayo inaweza kusababisha kifo au tatizo la kudumu.
Hawa ni vimelea wa jamii ya bakteria ambao wanajulikana kwa jina la escherichia coli (E.coli)
Bakteria hawa wanapatikana katika utumbo mpana lakini
husafiri kupitia njia ya haja kubwa kwenda katika njia ya mkojo na kusababisha maambukizi
katika kibofu na figo.
UTI
INAVYOENEA
- Tabia na mazingira
yanayoweza kusababisha maambukizi katika njia ya mkojo kuwa ni kushiriki ngono
mara kwa mara na watu tofauti bila kutumia kinga.
- Hali hii inamfanya
mtu kuchukua bakteria wa UTI kutoka kwa mwenzi wake ambaye tayari ana maambukizi
hayo.
- kujitawaza kutoka
nyuma kuja mbele baada ya haja kubwa kunapelekea maambukizi hasa kwa wanawake.
- Hii ni kwa sababu
vimelea hao hupatikana kwa wingi katika utumbo mpana. Hivyo, kitendo cha kujisafisha
kwa njia hiyo, huwasafirisha bakteria hao kutoka sehemu ya haja kubwa kuja
katika njia ya haja ndogo.
- mazingira haya
husababisha UTI kwa wanawake kwa sababu njia ya haja kubwa na ndogo zipo karibu
sana.
- Mama wajawazito
pia wako hatarini zaidi kwa sababu mimba
kukandamiza kibofu na kusababisha kukosekana kwa uwazi katika njia ya mkojo
ambayo kitaalamu inajulikana kama Incomplete emptying.
Takwimu nchini zinaonyesha
kuwa kwa kila wanawake watano, mmoja amewahi kupata ugonjwa huo.
Hali hiyo huweza kuwa ni
ya kujirudia mara kwa mara kwa baadhi ya wanawake, hasa kinamama wajawazito na watu
wenye umri mkubwa.
Mbali na wanawake kupata
maambukizi zaidi, watoto wa jinsia zote pia wako hatarini.
Ni vema mazingira ya chooni
na bafuni yawe safi ili kuwalinda watoto dhidi ya maambukizi haya.
Ø Maambukizi
katika njia ya mkojo yanaweza kusababishwa na bacteria, fangasi au virusi. Na matibabu
yake hutolewa kulingana na aina ya vimelea waliosababisha maambukizi hayo.
KISUKARI
HUATHIRI ZAIDI
- Maambukizi haya
yanaweza pia kuwaathiri watu wenye kisukari kirahisi zaidi kwa sababu ya sukari
nyingi iliyopo katika mkojo.
- Sukari hiyo
huchochea kuzaliana kwa bacteria wanaosababisha maambukizi.
- Kwa mujibu wa
ripoti iliyofanywa na Chama cha Kisukari Cha Marekani (ADA), asilimia 9.4 ya watu wanaokutwa na kisukari wanaugua
pia UTI wakati asilimia 5.7 ni wenye
maambukizi lakini hawana kisukari.
- Wenye kisukari
wanaathirika zaidi kwa sababu pia bakteria
kuzaliana kwa wingi na baadhi ya mishipa inaharibika na kushindwa kufanya kazi
yake ipasavyo.
- Hata hivyo,
ripoti hiyo imebainisha kuwa sukari nyingi iliyopo kwenye damu ya mgonjwa wa
kisukari inaua seli nyeupe za damu, hivyo mwili unakosa kinga ya kupambana
na bakteria hatarishi walioingia mwilini.```
ATHARI,
DALILI, TIBA
o
Endapo mtu hatatibiwa mapema au kumaliza
dozi, ugonjwa huu unaweza kuwa sugu na kusababisha kuharibika kwa figo na kibofu.
o
Maambukizi yanayotokea chini ya kibofu huathiri
kibofu na mirija inayotoa mkojo nje.
o
Maambukizi yanayotokea katika figo ni hatua
ya juu na athari zake ni kubwa zaidi kuliko athari zitokeazo katika mirija na kibofu.
o
Athari nyingine ni mwanamke mjamzito anaweza
kuzaa mtoto kabla ya wakati au mtoto kuzaliwa akiwa na uzito pungufu.
o
Wagonjwa huwa tunawashauri kupata tiba mapema
na kumaliza dozi na watoto wadogo na wazee pia wanaweza kupata maambukizi hayo kirahisi,
hivyo wapimwe mara kwa mara.
o
Ripoti
ya ADA inabainisha dalili za awali kwa
mtu mwenye maambukizi katika njia ya mkojo ni maumivu wakati wa kukojoa, kuhisi
kukojoa lakini ukienda chooni mkojo unatoka kidogo sana, kukojoa mkojo wenye damu
na maumivu ya tumbo na mgongo.
o
Dalili kwa maambukizi yaliyokomaa, zinaelezwa
kuwa ni homa kali, kutetemeka, kutapika, kuharisha na maumivu ya mgongo.
o
Hata hivyo, kinga ya ugonjwa huu inaelezwa
kuwa ni kuzingatia kanuni za usafi hasa baada ya haja kubwa na kujisafisha kuanzia
sehemu ya mbele kwenda nyuma ili kutoruhusu vimelea kuingia katika njia ya mkojo
kwa urahisi.
o
Inashauriwa kumwona daktari baada ya kuona
dalili hizi na kutumia kikamilifu dawa itakayopendekezwa na daktari.
o
Ni muhimu kwa mgonjwa kumaliza dawa ili kuzuia
kujirudia kwa ugonjwa huo mara kwa mara na kusababisha madhara au usugu```
Kwa ajili ya tiba na ushauri wasiliana nasi
No comments:
Post a Comment